Mfumo wa kisiasa wa Iran umejengwa juu ya nguzo imara ya Wilayat al-Faqih; mfumo ambao si tu mfano wa uongozi wa dola, bali pia ni dhihirisho la uhusiano wa moyoni na wa kiitikadi kati ya Umma na Kiongozi. Nafasi hii ni zaidi ya mfumo wa kawaida wa kiutawala; ni ngome ya uthabiti wa nchi mbele ya dhoruba kali za kisiasa na vitisho vya kutoka nje. Azma na mshikamano wa wananchi na mhimili huu wa uongozi wa Kiwilaya ni ukweli ambao hakuna shinikizo, vikwazo wala njama zilizoweza kuuvunja; kwa sababu mshikamano huu una mizizi katika imani ya msingi wa dini ambayo imefungamana kwa kina na roho pamoja na utambulisho wa Wairani, na hivyo kuendeleza upya azma ya kitaifa ya kulinda uhuru na heshima ya nchi.
Kwa muda wote ambao utiifu huu wa kujitambua na imani hii thabiti vinaendelea kuishi ndani ya jamii, matumaini ya kupatikana kwa uadilifu na uhuru nchini Iran pamoja na miongoni mwa wanyonge na waliodhulumiwa wote duniani yataendelea kubaki hai. Ustahimilivu huu, kwa hakika, umeunda kizuizi kisichopenyeka dhidi ya tamaa za kujitanua za kambi ya ubeberu na maadui wa ubinadamu. Katika mantiki ya muqawama, imani hii pamoja na matumaini ya pamoja ndivyo ambavyo vimekuwa kama mwiba machoni mwa wenye nia ovu, na mara kwa mara vimeharibu hesabu zao za kutaka kuyapigia magoti mataifa huru. Huu ni ukweli ambao umeifanya Iran kuwa kitovu cha kutoa hamasa kwa harakati zote za kudai haki katika pembe zote za dunia.
Maoni yako